GET /api/v0.1/hansard/entries/1385488/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1385488,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1385488/?format=api",
    "text_counter": 568,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa ruhusa kuchangia kuhusu Mswada huu unaohusu nyumba za bei nafuu. Kama kuna watu ambao hawafai kupinga ujenzi wa nyumba za bei nafuu ni Sen. Oketch Gicheru na Sen. Ledama. Mwaka wa 2005 nilikuwa pahali panaitwa Gogo kule Kisii na Migori ambako hakuna chochote. Serikali ya Kenya Kwanza ingeanza kujenga nyumba za bei nafuu kule kwa sababu hakuna tofauti kubwa kati ya Embu na Kisii. Kutokana na ujenzi wa nyumba, takriban watu 150,000 wameajiriwa. Hawa ni wavulana na wasichana wetu. Wengine ni washi, wengine ni mafundi wa umeme na vile vile kuna watu wa kusafisha. Kutokana na hiyo, viwango vya ukora mijini na vijijini vimepungua. Kwa hivyo, naunga mkono kwamba nyumba za bei nafuu ziendelee kujengwa katika kaunti zote. Takriban nyumba 2,000 zimejengwa katika kaunti nyingi. Naipongeza Serikali ya Kenya Kwanza kwa kazi inayofanya. Naomba iendelee hivyo kwa kipindi cha miaka mitano ya muhula wa kwanza kisha miaka kumi ya awamu ya pili. Ujenzi wa nyumba ukipelekwa katika sub counties, uchumi wa kaunti zetu utaimarika. Ningependa watu wajue kuwa sisi kama Maseneta huwa tunatembea sehemu tofauti tofauti. Kwa mfano, mimi nilikuwa Colorado, North Carolina na Dubai. Mambo niliyoona kule hayakuanza sasa. Utapata mtu analalamika kuanzia asubuhi hadi jioni anapolipa nauli ya Kshs100. Kule mtu anawezalipa kama Kshs200 kwa muda wa masaa mawili. Muda huo ukiisha inabidi uondoke. Naomba walio wengi na walio wachache tuungane pamoja ili tupitishe Mswada huu na kuwezesha Serikali kujenga nyumba za bei nafuu. Hiyo itatuwezesha kuimarisha uchumi wa nchi yetu ya Kenya. Ninawaomba wale walio wachache katika Bunge hili, watuunge mkono katika Serikaki ya Rais William Ruto na Rigathi Gachagua kwa hiki kipindi cha miaka mitano"
}