GET /api/v0.1/hansard/entries/1385524/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1385524,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1385524/?format=api",
    "text_counter": 604,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Jambo lengine ni hizi nyumba zitanufaisha Wakenya wetu. Niko katika Kamati ya Uchukuzi, Barabara na Ujenzi wa Nyumba. Watu wa matatu na jua kali walikuja kuleta mapendekezo yao kwa hii Kamati. Walisema ya kwamba itawasaidia ndugu zetu wahandisi, maseremala na waashi kupata kazi. Kwa hivyo, Mswada huu utawasaidia Wakenya kwa kuwapa kazi na nyumba ili watu wetu waache kuishi katika hali duni. Lakini, niliposikiliza ndugu zangu, wanasheria hawa wawili walipoongea, nilipigwa na butwaa kwa sababu tunaongelea kuhusu shida ya nyumba. Kwao, nyumba sio shida. Shida yao--- Bw. Spika wa Muda, maneno yananisumbua kwa sababu pengine hawa ndugu zangu hawajatembea mashinani waone shida za wananchi. Nimesikia ya kwamba, nyumba hizo hazijaanza kutengenezwa. Juzijuzi, tulikuwa mji wa Nanyuki na tayari nyumba hizi zimeanza kutengenezwa na vijana wanashukuru."
}