GET /api/v0.1/hansard/entries/1385994/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1385994,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1385994/?format=api",
"text_counter": 252,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Mheshimiwa Spika wa Muda. Nami naunga mkono Mswada huu ulioletwa Bungeni kuhusu maendelo ya idara za mikoa. Mengi yamesemwa, lakini licha ya kuwa tunataka maendeleo katika mikoa yetu… Pia nimeskia wenzangu hapa wakitaja mambo ya ukabila na mengineo… Katiba yetu ilileta ugatuzi ili watu waweze kufaidi kutokana na rasilimali zao. Katika Bunge hili, tunashuhudia unafiki mkubwa kwa sababu jamii ndogo ndogo hazijafaidika kisawasawa kutokana na rasilimali zao. Kwa hivyo, licha ya kuwa tunataka kuteua watu waliostawi na kuimarika kuongoza idara hizo, ili kusawazisha rasilimali na uchumi katika mikoa yetu… Lakini hata juzi baada ya kupiga kura, watu walioanguka kura wameteuliwa katika idara hizo. Hivi sasa, idara hizo hazina maana kwa kuwa tumeingiza siasa. Kila siku, ni siasa tu zinazopigwa katika idara hizo. Hata ukienda kutafuta usaidizi, unaambiwa kuwa wewe ni wa chama fulani. Walioanguka kura wajifunze kurudi kiwanjani tena. Sio tu walimbikizwe katika idara tofauti na hata hatujui wanachokifanya huko. Licha ya kuwa tunataka walio na uzoefu katika kuongoza idara hizo, ni lazima tuheshimu ugatuzi. Watu wanaotoka sehemu zile wanaelewa vizuri jiografia, tamaduni, mila na matatizo yanayowakumba wanachi wa sehemu hizo. Kwa hivyo, tunapaswa kuteua watu kutoka sehemu hizo, lakini wawe wamebobea katika nyanja zao, yaani, ni professionals. Nimeskia Mbunge mmoja akisema tuwache mambo ya ukabila, lakini tunashuhudia ukabila mwingi mno wakati wa kutafuta kura na katika nyanja zote nchini. Isiwe eti katika maendeleo, watu wanapouliza haki zao, wanalemezwa na ukabila. Sisi Wapwani tumefinyiliwa sana. Ukiangalia pale Pwani, watu wanaopewa kazi sio watoto wetu. Ndugu yangu, Mhe. Owen Baya, amezungumza kwa uchungu mwingi kwa sababu ya mambo tunayoyapitia kama Wapwani. Hatutetei ukabila, lakini tunasema kuwa mtu hucheza kwao, na hupata kile cha kwao. Tumefinywa sana kama Wapwani, na rasilimali zetu zinaenda sehemu zingine. Tumekaribisha kila mtu kwetu, hatukatai. Pia ni haki kwa watu kutoka sehemu zingine za Kenya kufanya kazi katika idara zilizoko Pwani. Lakini wasitufinyilie. Tusione watu wanaofaidi ni wale ya kutoka sehemu zingine, ilhali Wapwani tunabaki nyuma. Wengi wamemtafsiri vibaya ndugu yangu Mhe. Owen Baya, lakini ni kutokana na uchungu tuonaosikia kama Wapwani. Tunataka mtu akiteuliwa kuongoza idara kama ya Kenya PortsAuthority, aangalie watoto wa Kipwani. Katiba yetu inasisitiza 70 per cent . The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}