GET /api/v0.1/hansard/entries/1388608/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1388608,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1388608/?format=api",
    "text_counter": 1358,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Tabitha Mutinda",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika. Bw. Misati, Waswahili walisema, “ajuaye uchungu wa mwana ni mzazi.” Na waliimba wakasema, “mtoto sio nguo, utaomba mtu.” Niulize leo ndugu yangu, ni nini hicho kilichofanya mwanao, Dennis, ambaye ameishi miaka kumi na tatu Nairobi, auze biashara yake na akuletee zile fedha? Swali la pili, katika ile biashara yako ya M-pesa, katika zile transactions inaonekana ya kwamba ulituma zile elfu mia mbili hamsini na moja kutumia simu yako ya rununu. Ni nini ilifanya zile pesa zilizobakia, zile elfu mia mbili arobaini na tisa, lazima zipeanwe katika kitita cha pesa taslimu? Asante, Bw. Naibu Spika."
}