GET /api/v0.1/hansard/entries/1388629/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1388629,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1388629/?format=api",
"text_counter": 1379,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Naibu wa Spika, swali langu ni kwa Bw. Misati. Unaonekana mtu aliyekomaa. Huenda ukawa mzee wa kijiji au mzee wa kanisa. Tunajua kuna mambo ya wazee, familia na marafiki. Kuna mambo ya mtoto wako na bibi yake. Vile vile, kuna mambo yako na bibi yako, na kuna mambo ya Deputy Governor na kazi yake. Wewe kama mzee unafaa kuunganisha watu ili mambo kama haya yasifike hapa. Mambo kama haya kule nyumbani kwa sababu ya urafiki na mambo mengine ya familia. Wewe kama mzee, ulichukua hatua gani kuzuia mambo kufika kwa County Government na hatimaye hapa? Bibilia husema, watu wawili hawawezi kutembea pamoja kama hawajakubaliana. Sasa inaonekana kazi ya Deputy Gavana na mambo ya familia yako hatarani."
}