GET /api/v0.1/hansard/entries/1388637/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1388637,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1388637/?format=api",
    "text_counter": 1387,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu wa Spika, kwa kunipa fursa hii. Hili ni Bunge la kumbukumbu na tumekuwa na kikao kama hiki, tukijadili Hoja kama hii. Nakumbuka ya kwamba, maswali tunayopaswa kuuliza, ni ya ufafanuzi mahali ambapo hatujaelewa vizuri. Lakini, maswali yanayoulizwa, ni kama kwamba, sisi tayari tumekata kesi na mwelekeo ambao tunataka kuchukua. Bw. Naibu wa Spika, Spika mwenzako alisema vivyo hivyo ya kwamba, maswali tunayouliza yanapaswa yaelekezwe kwa ufafanuzi na si kuonekana kwamba tayari tumechukua msimamo na mwelekeo."
}