GET /api/v0.1/hansard/entries/1392352/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1392352,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1392352/?format=api",
    "text_counter": 264,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana Mhe. Mwenyekiti wa Muda, na mimi niweze kuchangia Mswada huu ambao umeletwa hapa. Sijui Bunge hili lilikuwa wapi wakati ule wakipitisha bila kurekebisha ndio hapa tuletewe tena waseme kuna marekebisho. Mimi bado ninapinga Mswada huu. Ikiwa yule ambaye anakatwa pesa yake ana shamba lake na hajengewi katika shamba lake, basi huu ni ulaghai. Huu ni wizi wa hali ya juu. Tuangalie tusiweze kufinya ugatuzi kwa sababu ikiwa jambo hili ni la kaunti, kwa nini wasiwachiwe hao wapange mikakati yao mpaka ije itokee huku juu. Wakenya bado mpaka sasa wanahangaika. Na mimi ninarudi pale pale. Ikiwa kweli Serikali inataka kujenga nyumba ambazo ni za watu wa mapato ya chini, ushuru unaokatwa kwingine unatosha."
}