GET /api/v0.1/hansard/entries/1392901/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1392901,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1392901/?format=api",
    "text_counter": 70,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Wundanyi, WDM",
    "speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
    "speaker": null,
    "content": "Kwa niaba ya wenzangu wa Pwani, mimi nikiwa mwenyekiti wa Vuguvugu la Wabunge wa Pwani, nachukua nafasi hii kuwakaribisha katika Bunge la Taifa vijana wetu kutoka Pwani, wajisikie wako sawa na wako kwao. Wajue sisi Wabunge wao tutafanya kazi ili masomo yao yasitatizike. Pia tutafanya kazi ili nchi yetu ipate nafasi za ajira wanapomaliza shule na vyuo ili wapate kazi na wabadilishe hali za maisha ya nyumbani kwao. Karibuni vijana wa COSAKU ambao ni wa kutoka Chuo Kikuu cha Kenyatta. Pengine niseme tu, nikiwa hicho chuo mwaka wa 1999 hadi 2003, mimi na wengine ndio tulianzisha Coast Students Association kule. Kwa hivyo, nikiwaona hapa, nafurahia, maanake najua kazi tuliyoifanya wakati ule, leo hii bado inabobea na bado wameshikilia umoja wa Pwani."
}