GET /api/v0.1/hansard/entries/1393000/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1393000,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1393000/?format=api",
"text_counter": 169,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nakuru County, UDA",
"speaker_title": "Hon. Liza Chelule",
"speaker": null,
"content": "Ni vizuri tutilie maanani maswala ya walemavu. Tunaishi na walemavu nyumbani kama dada, ndugu na majirani, na wengine tunashiriki nao kanisani pamoja. Wengi wao ni watu wanaowajibikia familia zao, na wanahitaji usaidizi. Walemavu wengi hawajajiandikisha katika makundi. Mara nyingi hata hawapati habari za kazi zinapotangazwa. Naomba Wabunge wenzangu tusimame na walemavu kuanzia ofisini mwetu. Ikiwa uko na ofisi ya Kiserikali au yako binafsi, ni vyema tuwapatie nafasi kama ilivyopendekezwa na Katiba. Ni kazi yetu, kama viongozi, kuwatetea walemavu. Tuelewe kuwa hawajiwezi kwa njia moja au nyingine. Lakini hiyo haimaanishi hawatafanya kazi. Tuwapatie nafasi katika maswala ya bursary na katika ofisi zetu."
}