GET /api/v0.1/hansard/entries/1393005/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1393005,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1393005/?format=api",
"text_counter": 174,
"type": "speech",
"speaker_name": "Magarini, ODM",
"speaker_title": "Hon. Harrison Kombe",
"speaker": null,
"content": " Ahsante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi kuchangia Riporti hii ya Kamati ya Mshikamano wa Kitaifa na Fursa Sawa. Kwa hakika, kati ya mashirika yaliokuja mbele ya Kamati, ni wazi kuwa kiwango cha walemavu kiko chini ya wastani unaohitajika na kupendekezwa na Katiba. Ulemavu sio ugonjwa. Haimaanishi kuwa walemavu hawawezi kufanya kazi. Hivyo, kuna haja ya kuwahushisha na kuwapa ajira katika nyanja zote. Kwa mfano, nimejumuisha walemavu katika kamati yangu ya NG-CDF na hata ofisini mwangu. Pia nimeona mlemavu akiwa katibu wa kudumu katika wizara husika katika Kaunti yangu. Tulipokumbwa na mafuriko huku Bate, Eneo Bunge la Magarini, Waziri huyo wa Kudumu alihusika vilivyo na kuhakisha kuwa waathiriwa walihamishwa na kupelekwa katika sehemu sawa, na pia wamepata chakula kutoka kwa wizara yake. Kusema kweli: “ Disability is not inability .” Walemavu wana uwezo wa kufanya vyema zaidi hata kuliko sisi tulio wazima. Hatufai kuwabagua kwa sababu Katiba imekataa ubaguzi kwa walemavu au mtu mwingine yeyote kwa sababu ya maumbile. Leo hii tuko wazima, lakini haimaanishi kuwa unavyozaliwa ndivyo unavyokua. Mara nyingi, tumeona ajali nyingi zinazowaacha watu wakiwa walemavu. Naomba Bunge hili liunge mkono Riporti hii ili tuweze kuwaweka walemavu mahali wanapostahili kama Wakenya wengine. Ahsante, Mhe. Spika wa Muda."
}