GET /api/v0.1/hansard/entries/1393059/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1393059,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1393059/?format=api",
"text_counter": 228,
"type": "speech",
"speaker_name": "Makueni County, WDM",
"speaker_title": "Hon. Rose Mumo",
"speaker": null,
"content": "Ulemavu ni jambo ambalo linahitaji kuzingatiwa sana Kenya, ili tuhakikishe kwamba walemavu wanapata nafasi. Katika ofisi yangu, nimepokea kesi nyingi za ubakaji wa watoto, na wengi wao ni walemavu. Wengi wao sasa wameanza kuingiliwa maana hawawezi kukimbia ama kufanya lotote. Walemavu wengi sasa wanakabiliwa na hatari kubwa kwa sababu hawawezi kukimbia au kujilinda. Wanaume wachokozi wanawalenga hasa watoto wa kike walemavu, na hii inahatarisha usalama wao. Tunahitaji kuhakikisha ya kwamba wanapata ulinzi unaofaa. Naunga mkono Ripoti hii na naamini kwamba jambo hili linahitaji kuangaliwa kwa dharura ili tuweze kuwasaidia wale wenye ulemavu. Mimi nilikuwa natembea vizuri lakini leo niko na ulemavu. Kwa hivyo, naelewa changamoto ya kutembea ukiwa mzima na ukiwa na ulemavu. Ni jambo ambalo lina shida sana na naomba kwamba watu waangaliwe. Pia, usajili wao uangaliwe kwa sababu wengi wanatafuta kupata kadi ya ulemavu na inakuwa shida kuipata. Kamati, nasema asanteni kwa hii Ripoti."
}