GET /api/v0.1/hansard/entries/1393097/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1393097,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1393097/?format=api",
    "text_counter": 266,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": {
        "id": 13383,
        "legal_name": "Ali Menza Mbogo",
        "slug": "ali-menza-mbogo"
    },
    "content": " Mhe. Spika wa Muda, nami ninasimama hapa kuunga mkono Ripoti hii. Nashukuru Kamati kwa kupanga mambo ya muhimu. Hii ni moja katika baraka ambazo mwenyezi Mungu atawapa neema kwa kukumbuka walemavu. Hata yule aliyeandika na anayesikiliza pia atapata baraka. Ndiyo maana tangu saa nane nimekaa hapa bila kutoka ili nami nipate neema hiyo ya kuwasaidia walemavu. Si kupenda kwa mtu kuwa na ulemavu au kasoro yoyote katika mwili wake. Ulemavu unaweza kumpata mtu yeyote ambaye sasa hivi anajiona mzima. Sote tunatumia vyombo vya moto, hivyo tunaweza kupatikana na jambo lolote wakati wowote na kuingia katika hali hiyo. Sheria zipo za kuwahifadhi, kuwasaidia na kuwalinda walemavu ila utekelezaji wa sheria hizo una shida. Kila mmoja wetu aliapa kuwa atailinda na kuitetea Katiba. Hivyo basi, ikiwa mtu hailindi, haitekelezi na haitimizi inavyosema, basi anapaswa ashtakiwe. Unaapishwa kusudi ushtakiwe unapokosea. Kwa hivyo, ikiwa halmashauri za Serikali haziajiri walemavu, mhusika ni lazima ashtakiwe kwa kuwa kinyume cha sheria kwa sababu aliapa kwa Katiba. Mhe. Spika wa Muda, pia majengo yetu yawe na urafiki na walemavu kulingana na ulemavu wao. Hapa kwetu Bunge kuna shida. Lazima turekebishe ili tuwe na urafiki na ulemavu. Leo kulikuja hapa shule ya walemavu inayoitwa, Thika School for the Blind. Walipanda ngazi, ambapo kungekuwa na lifti ingekuwa rahisi kwao kufika juu. Walipofika hapa, mmoja wao alizimia pale juu, kwenye Gallery ya Ukumbi huu. Ilibidi waletwe watu kutoka sehemu tofauti kama Shirika la Msalaba Mwekundu kumpa huduma ya kwanza. Ni vyema hata sisi katika Bunge hili tuwe na wafanyakazi ambao wanaweza kuzungumza kwa ishara na viziwi. Sharti nasi tuwe mbele katika kutekeleza vile Katiba inavyosema. Pia, Parliamentary Service Commission (PSC) iweze kuwaajiri wafanyikazi walemavu. Tusipowaajiri, wanakaa kule nje ama barabarani wakiombaomba. Si kupenda kwao! Ni kwa sababu wamekataliwa na kutengwa. Wakati wangu umekwisha na namshukuru Mwenyekiti wa Kamati. Lakini, ningesisitiza kwamba sheria itekelezwe ili walemavu waweze kuajiriwa kulingana na"
}