GET /api/v0.1/hansard/entries/1393733/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1393733,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1393733/?format=api",
    "text_counter": 163,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Bw. Spika. Nami najiunga na maoni yaliyotolewa na Kiongozi wa Walio Wengi, Sen. Cheruiyot, ya kwamba, kitambo kidogo, kulikuwa na pigeon hole ; mahali ambapo tulikuwa tunapata barua zinazotoka katika vitengo vya Serikali hususan Ofisi ya Controller of Budget. Tulikuwa tunapata nakala hizo na barua nyingine ambazo zilikuwa zinatuhitaji kwenda katika mialiko ya aina yoyote tuliyokuwa tunapata kupitia kwa hivyo visanduku ambamo barua zetu zilikuwa zinawekwa. Tokea sijui ni lini, sijaweza kuona hivyo visanduku vikitumika. Ni kweli kabisa ya kwamba visanduku hivyo huenda vimefungwa sasa. Tunaomba ya kwamba ikiwa inawezekana, kupitia uwezo wa Ofisi yako, Bw. Spika, ama unaweza kuamrisha vifunguliwe na iwapo kuna message zozote za Serikali, ama hususan maelezo ya matumizi ya katika kaunti zetu, ziwe zinawasilishwa kwetu. Mara nyingi, itaonekana kama Maseneta wanaingilia taratibu za ufanyikazi katika kaunti zetu. Lakini utaona ya kwamba majukumu ambayo tumepewa sisi kama Maseneta, ya kuangalia kwamba pesa zinatumika kwa njia nzuri, inakuwa dhaifu sana ambapo hatuwezi kupata nafasi kubwa isipokuwa kutegemea ripoti kama hizi. Ingekuwa vyema ikiwa tutapewa nafasi hiyo ili pia sisi tuwe tunaangalia, kuangazia na kuwarekebisha wale wanaoongoza kaunti katika majukumu ya kutumia pesa. Kuna pesa zinazotumika kiholela; pesa zinatumika kwa njia ambayo pengine sio nzuri lakini ikiwa tutapata nafasi kama hiyo, tunaweza kuwaeleza wale ili wafikirie ya kwamba sisi tunawachunguza ama tunataka wachukuliwe hatua. Tunataka kuona ya kwamba pesa ambazo zinaenda mashinani zinatumika kwa njia nzuri; pesa zinazoenda mashinani zinatumika vile zinavyotakikana. Ombi langu ni kwamba hivi sasa tuwe na uhusiano mwema na Ofisi ya Controller of Budget ili aweze kutuletea ripoti na hatua ichukuliwe mara moja."
}