GET /api/v0.1/hansard/entries/1393747/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1393747,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1393747/?format=api",
"text_counter": 177,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, ukweli wa mambo ni kwamba Serikali Kuu imejitolea ili wakulima wapate pembejeo kwa bei nafuu. Hili ni jambo nzuri lakini pembejeo yafaa ipelekwe mahali wakulima wako huko vijijini. Pembejeo hii hupelekwa mijini na huku wakulima wengi hawako mijini. Kwenye Kaunti ya Laikipia, pembejeo hii haifikishwi mashinani, inafaa ipelekwe maeneo ya Sipili, Matanya na Salama mahali wakulima wako. Isipelekwe mijini ambapo wakifikisha mijini wanasema pembejeo imefikishwa kwa wakulima. Ni kinaya kwa sababu tunaongea kuhusu pembejeo. Lakini ninaunga mkono Taarifa ya Sen. Wafula kutoka Bungoma. Pembejeo hii ikiletwa kwenye huu msimu wa mvua, Seneta amesema kuwa hakuna mahindi ya kupanda; ni vizuri tuwe na mbegu kwa sababu huu ni msimu wa kupanda. Wakulima wanahitaji mbegu ambazo zimefanyiwa utafiti, kwenye bei nafuu na mazao yake yataleta mavuno ambayo wananchi wa Kenya watafurahia. Serikali imeahidi kupunguza gharama ya maisha. Gharama hii itapungua tukipata mbegu ambazo zimekubalika na kufanyiwa utafiti wa kisayansi ili kuleta mavuno mazuri. Naunga mkono na kushukuru kwa kunipa fursa hii. Asante."
}