GET /api/v0.1/hansard/entries/1394116/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1394116,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1394116/?format=api",
    "text_counter": 271,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Murkomen",
    "speaker_title": "The Cabinet Secretary for Roads and Transport",
    "speaker": {
        "id": 440,
        "legal_name": "Onesimus Kipchumba Murkomen",
        "slug": "kipchumba-murkomen"
    },
    "content": " Bw. Naibu wa Spika, ni kweli kwamba nilisema kwa muda wa wiki mbili, mwanakandarasi huyo atakuwa amerejea kuendelea na kazi kwenye barabara kutoka Ngong kuelekea Suswa. Kutokana na sababu ambazo nimeeleza hapo awali – inahusiana na mambo ya fedha, hasa bajeti – hatukuweza kumrudisha mwanakandarasi yule kwa sababu licha ya kuwa hatukuwa tumemlipa Kshs600 million, alihitaji zaidi ya pesa iliyowekwa kwa bajeti. Ilitubidi tuendelee na mazungumzo. Tuna imani kwamba hivi karibuni, mwanakandarasi huyo atarejea barabarani. Nachunga ulimi wangu kwa sababu sitaki kurudia kusema wiki mbili, licha ya kuwa alikuwa amekubali kurudi kwa muda wa wiki mbili. Lakini tulipata shida baada ya muda wa kandarasi kwisha na sasa tumefanya mkataba na contractor na atarudi barabarani. Bw. Naibu Spika, ningependa kutumia nafasi hii kumpongeza Sen. Olekina kwa sababu amesimama kidete kwa masuala ya barabara hii."
}