GET /api/v0.1/hansard/entries/1395235/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1395235,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1395235/?format=api",
    "text_counter": 91,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Bw. Spika, nasimama kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu Kipengele 53(1) kuomba Taarifa kutoka kwa Kamati ya Ardhi, Mazingira na Mali Asili kuhusu uharibifu na uchafuzi wa mazingira kutokana na uchimbaji wa madini ya chuma katika eneo la Jaribuni, Kauma, Kaunti ya Kilifi. Katika Taarifa hiyo, Kamati hiyo inafaa kuangazia yafuatayo- (1) Kuchunguza uharibifu wa uchafuzi wa mazingira na athari za afya zinazotokana na uchimbaji wa madini ya chuma katika eneo la Jaribuni, Kauma, unaotekelezwa na Kampuni ya China inayoitwa Wu Ying. (2) Ieleze hatua gani Wizara ya Madini na Uchumi Samawati na Mamlaka ya Kitaifa ya Usimamizi wa Mazingira (NEMA) zimechukua kuhakikisha usimamizi wa matumizi sahihi katika uchimbaji wa madini eneo hilo la Jaribuni, Kauma, kwa lengo la kuboresha maisha na mazingira ya wakazi wanaoishi sehemu hizo. (3) Kubainisha wazi hatua ambazo kampuni ya China inayoitwa Wu Ying, chini ya wajibu wake wa kijamii (Corporate Social Responsibility), imechukua katika jitihada za kupunguza athari mbaya zinazotokea katika uchimbaji wa madini ya chumba katika eneo hilo la Jaribuni. (4) Ipendekeze hatua zitakazochukuliwa kuzuia utegemeaji wa uchimbaji madini unaochangia pakubwa uharibifu wa mazingira na uchafuzi katika maeneo hayo."
}