GET /api/v0.1/hansard/entries/1395282/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1395282,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1395282/?format=api",
"text_counter": 138,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Nasimama kuunga mkono Kauli iliyoletwa na Kiongozi wa Walio Wachache, Sen. Madzayo. Kampuni zinapaswa ziwe nyingi. Tukiwa na kampuni nyingi nchini tutaimarisha uchumi wetu. Kampuni hizi ambazo zinakuja zisiwe ni chanzo cha kuharibu mazingira na kuangamiza wananchi wa Kenya. Nimemsikiza kiongozi wa Walio Wachache akisema ya kwamba kuna kampuni ya Uchina ambayo kazi yake ni kuchimba madini. Baada ya kuchimba madini, inaharibu mazingira yetu. Hivi juzi tu tulikuwa na kongamano kubwa katika Jamhuri yetu ya Kenya na tukasema ya kwamba sisi tuko katika mstari wa mbele kusema tunapaswa kulinda mazingira yetu. Lakini ni kinaya wakati sisi tunaposema hayo maneno na unapata ndugu zetu kutoka Kilifi wanaendelea kusononeka na kupata taabu kwa sababu ya hizi kampuni ambazo hazisumbuki au kuangalia watu ambao wanaishi katika sehemu zile. Bw. Spika, nilikuwa nikifuatilia hili jambo kwa sababu niliona mambo haya yakiangaziwa katika vyombo vyetu vya habari. Nilipoangalia, niliona ya kwamba mahali hawa wananchi wanaishi, wale waliyo karibu na ile kampuni, hata baada ya wao kuathiriwa na yale mambo ambayo yanatendeka pale; watu wamepata kifua kikuu na sehemu ile hata haina zahanati. Watu wanawachwa kuendelea kusononeka na kupata taabu. Ndio tunaunga mkono kuwa na kampuni, lakini hizi kampuni zisiwe ndizo chanzo za kuangamiza wananchi wetu. Kwa hivyo, hizi kampuni ama idara ambazo zinapaswa kuhusika kuangalia hayo mambo kama hii idara ya National Environmental Management Authority (NEMA), inatupa kiwewe kwa sababu ikiwa inapaswa kushugulikia mambo haya, inapatia hawa watu leseni namna gani, ilihali hawa watu wanaendelea kuharibu mazingira yetu? Ndio tunataka uchumi lakini tusije tukaharibu mazingira yetu tukiwa tunazingatia mambo ya uchumi. Naunga mkono taarifa iliyoletwa na kiongozi wa Walio Wachache na ninamwambia ashikilie papo hapo ndio Wananchi kutoka Kilifi wasipate shida. Kwa sababu, watu wa Kilifi wakiwa na shida, hata wananchi wa Laikipia wanapata shida kwa sababu ni marafiki. Sisi ni ndugu wa kufa kuzikana. Asante."
}