GET /api/v0.1/hansard/entries/1395293/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1395293,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1395293/?format=api",
"text_counter": 149,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante Bw. Spika. Naunga mkono Taarifa iliyoletwa na ndugu yangu, Seneta wa Kaunti ya Meru, kuhusu kushikwa kwa Sniper. Sio kushikwa peke yake, bali kutolewa ndani ya nyumba na watu ambao hawajui, waliojitambulisha kwa familia na yeye mwenyewe, halafu wakamueka kwa gari na kupotea naye. Vitendo kama hivi vimetendeka sana na vimefanywa katika mikono ya polisi. Watu wanakuja kwa nyumba, wakishajitambulisha kwamba wao ni polisi, wanatoa mpaka vitambulisho na wanabeba mtu wanaenda naye. Hatimaye, tunaona huyo mtu anapatikana ametupwa mahali fulani baada ya siku fulani akiwa amekufa. Tabia kama hizi, hivi sasa zimeanza kuzidi kwa sababu si Meru tu ambapo kitendo kama hiki kimetokea kwa waandishi wa habari wa mitandaoni ama bloggers ."
}