GET /api/v0.1/hansard/entries/1395297/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1395297,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1395297/?format=api",
"text_counter": 153,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "wenu. Hiyo imetendeka kila mahali katika nchi. Hata upande wa Pwani, kule Mombasa, kuna blogger anayejulikana sana, anaitwa Yusuf. Polisi walienda nyumbani kwake na kumchujua. Watu walijitambulisha kwa familia yake kama polisi. Hatimaye, baada ya siku fulani, alipatikana katika hali ambayo si sawasawa. Alikuwa amepigwa risasi na ameuawa. Bw. Spika, ikiwa hawa watu wamekuja ndani ya nyumba na kujitambulisha kama polisi, itabidi sasa tuanze kukataa na wapendwa wetu. Tusiwaruhusu waende nao kwa sababu tunajua wakienda nao, mwishowe tutapata miili ya wapendwa wetu katika vichaka; wapatikane ama wasipatikane. Tabia kama hizi zimekuwa zikitendeka sasa baada ya mda mfupi. Njia inayotakikana kufanyika ni kwamba polisi wakome kupoteza Wakenya. Tunajua kuna sheria. Wakishika watu ni lazima wapelekwe kortini, waende washtakiwe, halafu mahakama ichukue mkondo wake. Akipatikana na hatia, hatua iweze kuchukuliwa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}