GET /api/v0.1/hansard/entries/1395311/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1395311,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1395311/?format=api",
    "text_counter": 167,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Shakila Abdalla",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 380,
        "legal_name": "Shakila Abdalla",
        "slug": "shakila-abdalla"
    },
    "content": "Bw. Naibu wa Spika, sharia na sheria hazina tofauti. Ni jinsi tu unavyopenda kutamka. Ukitaka kusema sharia ama sheria, inamaanisha kitu kimoja. Ukitaka kujua zaidi, nione nyuma ya tent nikufunze mengi. Bw. Naibu wa Spika, katika nchi kama Rwanda, boda boda hubeba mtu mmoja na wote huvaa helmet . Hapa Kenya, boda boda inaweza kubeba watu wanne au watano na wakianguka, wote wanafariki kwa sababu hawafuati sheria za kuvaa helmet zinazozuia mtu kuumia endapo atapata ajali. Ni muhimu law enforcement itekelezwe ili kupunguza ajali za barabarani. Utakuta polisi wa trafiki wanachukua hongo barabarani. Akikuta scratch kwa gari lako, anakuuliza mbona limekwaruzwa na kwa hivyo unafaa kutoa kitu kidogo. Hawaelewi hata kama gari lina shida. Ni njia gani itakayochukuliwa na Serikali kuhakikihsa kwamba magari yanayoendeshwa barabarani yako sawa na salama? Utakuta magari mabovu yanaendeshwa barabarani. Hayo ndio yanayochangia ajali. Utakuta gari halina breki---"
}