GET /api/v0.1/hansard/entries/1395339/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1395339,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1395339/?format=api",
"text_counter": 195,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Olekina",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 407,
"legal_name": "Ledama Olekina",
"slug": "ledama-olekina"
},
"content": "Asante Bw. Naibu wa Spika kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia Kauli ambayo imeletwa na Seneta kutoka Kilifi, inayohusu uchimbuaji wa madini katika eneo la Jaribuni Kilifi County. Uchimbaji wa madini ni jambo ambalo linahitaji kuzingatiwa kwa umakini sana. Wakenya huwa hatuzingatii mazingira. Lile tunalozingatia sana ni la uwekezaji. Inatubidi sasa tuweze kuangalia jambo linalotukera sana. Sisi kama wawakilishi wa Wakenya tunapigiwa simu kuulizwa tutume pesa ili iweze kupeleka watu hospitalini. Bw. Naibu wa Spika, ukisafiri hivi sasa kutoka Nairobi uelekee Kaunti ya Kilifi, eneo la Jaribuni, utakuta kwamba hali ya afya ya Wakenya wanaoishi kule imezoroteka vibaya sana. Ningependa kumshawishi Kiongozi wa Walio Wachache kuwa angeleta hoja hapa ili kazi inaloendelea huko iiweze kusimama. Huyo mwekezaji wa hii kampuni inayoitwa China Wu Yi Company ingelazimika awache uchimbaji huo wa madini hadi masuala ya kijamii yashughulikiwe. Ni aibu sana kwamba jambo ambalo sisi kama Wakenya tunatilia maanani ni kuwa matajiri sana. Mwekezani huyo amekuja huko kuchimbua madini, ametoa chuma, akauza na kupata pesa. Ila amewacha wananchi wale wanaishi katika eneo hilo ya Jaribuni mahospitalini. Wakienda hospitali hawapati dawa. Hii ni nchi gani tunatengeneza? Hili ni jambo linalonikera sana kwa sababu hata ukienda kule Narok uteremke mahali kunaitwa Siabei, kuna boma ya watoto ambao hawana familia. Chini yake kidogo kuna shimo kubwa lililoachwa na wale waekezaji ambao pia walikuwa wanachimbua madini, mchanga na mawe ya kutengeneza mabarabara. Je, ni siku gani sisi kama wawakilishi wa Kenya tutakasirika tuweze kuwaweka Wakenya wetu mbele na maneno ya wawekezaji yawe ni kitu cha baadaye? Itakuwa ni haki kweli tukiwa na waekezaji wengi lakini hatuna Wakenya ambao wanaweza kuishi na kufaidika kutokana na mambo yale waekezaji wanaleta? Mhe. Madzayo ameuliza jambo ambalo pia mimi ningependa kuuliza, kuhusu majukumu ya Mashirika ya Kijamii au Social Corporate Responsibility (CSR). Mara nyingi hata sisi hapa tukizungumza, tunajiuliza haya majukumu ya kijamii ni gani? Hii kampuni sijui inaitwa China Wu Yi imeweza kusema hili ndilo jukumu letu na tutahakikisha ya kwamba wananchi wa hapa wamepata matibabu wakigonjeka? Uchimbaji wa madini hasa chuma ama iron ore inaleta magonjwa mabaya sana. Hata ile pofu yake pamoja na ile inabaki baada kuosha ile chuma ikianza kutiririka chini, inaleta magonjwa kama vile saratani na wananchi wa Kilifi wanaendelea kuangamia. Hili ni jambo sasa kama Seneti ya Kenya ni lazima tujiulize kweli ni haki wananchi wa Kilifi waendelee kuangamia? The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}