GET /api/v0.1/hansard/entries/1395419/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1395419,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1395419/?format=api",
"text_counter": 275,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ninafurahi kuwa Maseneta wengi wamechangia kuwe na ripoti za mara kwa mara ambazo zinakuja hapa kutoka kwa Hazina Kuu ya Kitaifa kwa sababu tukiletewa Mswada kama huu wa kuangalia mipango ya deni na mikopo ya Serikali hatuiangalii tena hadi mwisho wa mwaka ujao. Mwaka ujao mwezi wa pili, tarehe 15 ndio tutaletewa Medium Term Debt Strategy (MTDS) nyingine ili tuiangalie upya. Hatuna ufuatilizi kuhakikisha kuwa yale ambayo yamependekezwa na serikali yanatakelezwa na kuhakikisha kuwa deni inabaki chini ya asilmia 55. Tulikubali mwaka jana kubadilisha mfumo wa deni kutoka kwa kiwango cha juu cha Kshs10 trilioni ambacho kilikuwa na tukaelekeza kiwe ni asilmia ya mazao katika nchi yani Gross Domestic Product (GDP). Hatari ni kuwa kwa sasa tuko asilimia 67.9. na kuna uwezekano wa kuenda juu kwa sababu tumeipa Serikali mpaka mwaka 2028/ 2029 ili iweze kupungua na kufika asilmia 55. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}