GET /api/v0.1/hansard/entries/1395422/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1395422,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1395422/?format=api",
    "text_counter": 278,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Baada ya miezi tatu Hazina Kuu Ya Kitaifa inafaa kuleta ripoti katika Bunge hili kueleza kiwango cha deni kimefika wapi. Sen. Mandago alizungumza kuhusu orodha ya madeni ambayo tunadaiwa. Hii ni muhimu sana. Deni zingine labda zilichukuliwa wakati wa nchi hii kupata uhuru miaka 60 iliyopita na labda tunayalipa. Mengine yalichukuliwa lakini hakuna miradi iliofanyika kwa mfano deni la Kimwarer na Aror dams. Wakati Rias alipokuwa Niabu wa Rais alisema kuwa Kshs7 bilioni zilipotea. Hizo si pesa kidogo. Tumeona kwamba Kaunti zetu kwa mfano Kaunti ya Mombasa inapewa Kshs7 bilioni mwaka mmoja kutoka kwa Hazina Kuu ya Kitaifa -"
}