GET /api/v0.1/hansard/entries/139558/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 139558,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/139558/?format=api",
"text_counter": 592,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, Wizara hii imetoa leseni kwa vyombo vingi vya kutangaza habari katika lugha mbalimbali hapa nchini. Ningependa ihimishe vyombo hivo kuwa na vipindi maalum katika Lugha ya Kiswahili. Ni kupitia vyombo hivi ambapo tunaweza kuwa na umoja wa taifa na kuwaunganisha Wakenya wote.Wakati huu, vyombo hivi vinatangaza katika lugha za kiasili. Lugha hizo nyingi haziwezi kuwaunganisha watu wetu. Ni lazima vyombo hivi vitumie lugha ya taifa ambayo itawaunganisha wananchi wetu. Ikiwa vitaendelea kutumia Lugha ya Kiingereza, ni wananchi wachache ambao wataelewa ujumbe wa viongozi wao. Si vizuri kwa sisi kama viongozi kutumia Kiingereza katika mikutano yetu ya kisiasa au wakati wa mazishi. Tukifanya hivo, ni watu wachache ambao hufahamu ujumbe wetu. Lugha ya Kiswahili imewaunganisha Watanzania. Hii ndio lugha ya taifa la Tanzania. Watanzania wote ni ndugu kwa sababu ya lugha hii. Vyombo vingi vya habari hapa nchini vinamilikiwa na watu watatu. Nikiwa na mpango wa kuanzisha chombo changu cha habari ni lazima nipate leseni kutoka kwao."
}