GET /api/v0.1/hansard/entries/139562/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 139562,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/139562/?format=api",
    "text_counter": 596,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, idhaa yetu ya Kenya Broadcasting Corporation (KBC) ndio inayopokelewa katika nchi yetu tukufu. Mimi ninatoa mwito kwamba idhaa hii iweke vipindi ambavyo vinahubiri utu na umoja wa Wakenya. Walete watu ambao wanazungumza na wananchi kule mashinani na waambiwe kwamba wasidanganyike na vyongozi. Wasidanganywe na viongozi ambao wanawazungumzia kwa misingi ya kikabila na kusema kwamba wao wakiwa Rais ndiposa hao watu watafaidika. Ni vyema kuwe na watu wa kukanusha mambo hayo kwa haraka sana. Ikiwa kiongozi fulani ameongea na kuzungumzia mambo ya kikabila, hiyo idhaa ya Kiswahili iwe imara na kukanusha mambo hayo kwa haraka na kusema kwamba aliyezungumza ni mharibifu na anagawanyisha nchi yetu na hafai kuongea mambo kama hayo. Tukifanya hivyo, tutakuwa tunaunganisha nchi yetu. Kupasha habari katika nchi na ile habari ambayo inasikizwa na wananchi ni lazima iwe ni habari ya kujenga na wala sio kuharibu."
}