GET /api/v0.1/hansard/entries/1398375/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1398375,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1398375/?format=api",
    "text_counter": 25,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu wa Spika, kwa nafasi hii. Jambo linalotokota mikononi mwako linahusisha umiliki wa ardhi ya watu wa eneo hilo. Ardhi ni jambo lililoleta mtafaruku na shida miongoni mwa Wakenya. Ukiangalia jamii ya Wamaasai, ulisikia juzi katika Seneti kwamba kuna zogo kati ya wakaazi wa Narok, Kajiado na Machakos, na pia maeneo mengi hapa nchini. Hao walioleta Ardhilhali hii hapa Seneti, kuna uwezekano kwamba wamejaribu kufuata nyenzo tofauti za Serikali kutafuta haki, lakini kwa sababu ya mirengo ya kisiasa au kitabaka na wale wanaohusika katika Serikali, hawajapata nafasi ya kumiliki ardhi yao. Ni jambo zuri wameleta Ardhilhali hii hapa na tunatarajia kwamba Kamati ya Ardhi, Mazingira na Maliasili hapa Seneti na kamati zingine husika, zitaweza kuhusishwa na kuleta mwafaka na haki miongoni mwa wakaaji wa eneo hilo. Bw. Naibu wa Spika, natarajia katika awamu hii ya Serikali ya Kenya Kwanza, tutafunga ukurasa huo wa watu kunyakua ardhi ya wengine pasipo kuheshimu sheria za nchi ya Kenya. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}