GET /api/v0.1/hansard/entries/1398382/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1398382,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1398382/?format=api",
"text_counter": 32,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii. Ninaunga mkono Ardhilhali hii ambayo imewasilishwa katika Seneti. Ni dhahiri shahiri ya kwamba mahakama imeamua na kutoa maamuzi kuhusu jambo hili. Ni vizuri ijulikane kwamba kamati itakayoshughulikia jambo hili, kwanza ishughulikie maamuzi ya mahakama kwa kuwa kulikuwa na fidia tayari na mahakama imesema kuwa wanapaswa kupewa zaidi ya Ksh170 milioni. Ni jambo la kuvunja moyo sana ikiwa waigizaji watakuja na kuwatimua watu mahali walikuwa wanaishi kwa muda mrefu kisha baadaye kuwaita maskwota. Ijapokuwa ni walala hoi, wana haki kisheria kumiliki ardhi hii. Uamuzi wa mahakama unastahili utiliwe maanani. Watu hawa wafidiwe pesa hizo wameitisha. Vile vile, tunataka wapewe nafasi ya kumiliki shamba hilo kwa sababu ni lao. Sijafuatilia maamuzi ya mahakama lakini kwa sababu nchi hii yetu mahakama ikifanya uamuzi, hatuna budi kuzingatia uamuzi huo. Bw. Naibu wa Spika, Seneti hii imeenda mahakamani wakati sheria zingine zimepitishwa na hazikufuatilia mwelekeo ambao unapaswa. Mahakama iliamua kwamba sheria hizo zirudishwe katika Bunge hili na ziweze kuangaziwa upya. Ikiwa hilo linaweza kufanyika, vile vile, hawa maskwota wanapaswa kupewa haki yao kulingana na uamuzi wa Mahakama. Asante."
}