GET /api/v0.1/hansard/entries/1398388/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1398388,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1398388/?format=api",
    "text_counter": 38,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu wa Spika, kwa kunipa fursa hii. Kweli, mimi kama area Senator wa Kaunti ya Kwale, shida hii imefika kwa wakati mzuri sana na imefika pahali pake. Mwanzo, mimi ni area Senator na pia mwanachama wa Kamati ya Ardhi, Mazingira na Maliasili. Hawa watu wa KISCO wamekuwa wakidhulumu watu wa Kwale Kaunti. Watu wameishi pale kwa miaka mingi na familia zao lakini leo wamekuwa maskwota ambao hawatambuliki. Wamesema watakatia wananchi wa Kwale ardhi ya sehemu fulani ili waweze kuishi lakini wamegeuka wakati amri ya mahakama imetoka. Sina maneno mengi ila kusema kwamba hii Ardhilhali ikifika katika kamati ambayo inahusika, ambapo mimi kama mwanakamati wa Ardhi, Mazingira na Maliasili ikiongozwa na Sen. Methu, Vice-Chairman - Sen. (Dkt.) Lelegwe na wanakamati wenzangu, nitahakikisha kwamba haki ya watu wa Kwale imepatikana kwenye hii shamba ya KISCO. Bw. Naibu wa Spika, itakuwa jambo mbaya sana kuonekana kwamba wananchi walioishi pale miaka mingi na mahakama imeamua wapewe ardhi hii, leo hawatambuliki. Hii tunahakikisha katika kamati ya Seneta Methu--- Najua utatoa mwelekeo kuhusu ni wapi Ardhilhali hii itaenda katika kamati gani. Nina imani Ardhilhali hii itaenda katika Kamati ya Ardhi, Mazingira na Maliasili. Samahani najuaa wazi. Kwa hivyo nawahakikishia wakazi wa Kwale wakinitazama katika runinga saa hizi, wasitie wasiwasi. Nitasimama imara---"
}