GET /api/v0.1/hansard/entries/1398419/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1398419,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1398419/?format=api",
    "text_counter": 69,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Miraj",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii nitoe mchango wangu. Kwanza, nakubaliana na walioleta Ardhilhali hii hapa yasikizwe. Zaidi, ningependa Bunge hili au taasisi husika ya NLC watuelezee sisi watu wa Pwani maana ya watu walio dhulumika kihistoria. Tunapozungumza hivi sasa, kule Mombasa, Tume ya NLC inazunguka na inahadaa wananchi wangu wa Mombasa. Haiwezekani kwamba mtu ambaye aliyekuwa Meya wakati huo; wenyeji wanamwita Liwali, alipewa mamlaka ya kusimamia wananchi wa Pwani. Akakabidhiwa ardhi awe msimamizi wa wanaoishi Mombasa. Leo hii amechukua ardhi ile akawaridhisha vizazi vyake. Leo hii watu wa Mombasa wameambiwa watakwenda kununua ardhi na mashamba ambayo ni yao kutoka kwa watu ambao wanaishi ughaibuni. Nataka kujua, ikiwa Seneti ni mbwa ambayo haina meno ama ni Bunge ambalo linatendea haki wananchi wa Kenya. Wakaazi wa Mombasa hawawezi kununua mashamba kwa watu ambao wamewanyang’anya. Hata ikiwa Rais ametangaza kuwa hakuna mtu atavunjiwa nyumba, sioni kwa nini ushuru wa Wakenya uchukuliwe upewe wale watu ambao wamewadhulumu wananchi wa Mombasa mashamba yao. Nazungumza hapa kwa uchungu mwingi kwa ile way forward ambayo NLC wamepeana kusema ya kwamba sisi watu wa Mombasa hatukudhulumiwa. Nataka leo tuambiwe ya kwamba ni nini maana ya historical injustice ili tuweze kujua. Hatutakubali---"
}