GET /api/v0.1/hansard/entries/1398448/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1398448,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1398448/?format=api",
"text_counter": 98,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. M. Kajwang",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13162,
"legal_name": "Moses Otieno Kajwang'",
"slug": "moses-otieno-kajwang"
},
"content": "Kwa hivyo, tuko team moja na tunashirikiana vizuri sana tukiwakilisha wakaazi wa Kaunti ya Homa Bay katika Bunge hili. Ningependa niwakaribishe wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kenyatta kutoka Ndhiwa. Ningependa niwahimize wasijione kama watu wa Ndhiwa pekee au kama Wajaluo lakini, wajione kama Wakenya. Hii ni kwa sababu wakija hapa Seneti, hata ingawa tunayo tofauti za kisisasa kule nje, wakati tukiwa hapa Seneti, tunawakilisha majimbo yote 47 na sisi sote tunafanya kazi kuhakikisha ya kwamba ugatuzi unafaulu na unaleta manufaa na matunda kwa vijana wetu. Ningependa pia niwahimize wafanye kazi kwa bidii na wajue uongozi sio kwa siasa peke yake. Wanaweza kuwa viongozi kanisani na professional settings---"
}