GET /api/v0.1/hansard/entries/1398577/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1398577,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1398577/?format=api",
    "text_counter": 227,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika wa Muda, naunga mkono Mswada wa wakulima wa miwa. Miwa hutengeneza sukari. Mimi ni naibu mwenyekiti katika kamati inayohusika na kilimo. Bw. Spika wa Muda, tulipokuwa tunazungumza juu ya mambo haya, sisi hatukuwa tunaichukulia kuwa ni kitu cha haraka kwa sababu siku hizi Serikali ya Kenya Kwanza inaongea kuhusu mambo ya “pesa mkononi” ama “pesa mfukoni.” Sisi tumeenda tukaita watu ili watupe maoni yao. Kuhusu mambo ya miwa, karibu kaunti 12 huwa zinapanda miwa, nayo sukari inatumika na Wakenya wote na hata nchi zingine duniani. Tuliangalia mambo mengi kama vile Sen. Osotsi amesema. Tuliona ni vizuri kwa wale watoto wa university ambao wanajua mambo ya Wizara ya Kilimo wanaweza kuenda pale kufunza watu na pia kujifunza vile mambo ya kutengeneza sukari yataendelea. Jambo lingine tuliangalia ni kuwa tungependa mtu kutoka nje atengeneze kampuni yake Kenya. Tukaonelea kuwa ni vizuri kwa sababu watu wengine ni matapeli ambao wanaweza kuondoka na pesa ya watu wa Kenya. Tukaangalia na kuona kuwa ni vizuri yule anayekuja kuweka kampuni yake hapa Kenya, kuwe na watu kama directors ambao watafanya kazi katika hiyo kampuni yake. Pia tuliona kuwa miwa ni kitu muhimu sana na wakati tulipokuwa wachanga, tulikuwa tunasikia vile miwa ilikuwa inasaidia serikali ya Kenya, lakini siku hizi watu wamenyanyaswa. Familia nyingi haziwezi kupeleka watoto wao shuleni na hata watu wanapokuwa wagonjwa, hawawezi kupelekwa hospitalini. Familia nyingi zimeachwa kuwa maskini kwa sababu matapeli waliingilia mambo ya kilimo ya miwa. Miwa inapopandwa, huwa inakaa mwaka mmoja na miezi nane kabla ya mavuno. Ni aibu sana kuwa kwa hizo kaunti zote, kwa sababu kazi yao ni kulima miwa, hali ya vile wanavyoweza kupandisha uchumi yao haionekana vizuri. Vile vile, chakula na maji imekuwa ni shida na hata shule na hospitali zote zimesambaratika kwa vile wanavyoumia. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}