GET /api/v0.1/hansard/entries/1398578/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1398578,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1398578/?format=api",
    "text_counter": 228,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Tuliangalia mambo mengi, sio eti tu tulienda kuita watu tukae pamoja tupitishe. Nimesikia watu wengine wakisema kuwa hawakuweko, kama vile Senator wa Nandi. Lakini kusema ukweli, sisi tulipoenda kule Nandi, watu wa Nandi walikuwa pale lakina Seneta wa Nandi hakupatikana. Mnavyojua huwa anakuwa na kazi nyingi huko nje. Labda alikuwa anafanya kazi ya kuharibia watu majina na tunajua kuwa kama hajahusishwa kwa jambo lolote, yeye huwa anapinga. Seneti inafaa kuunga mkono mambo ya sukari. Sio tu kwamba sisi Wanakamati wa Kamati ya Kilimo tulienda tukaandika mambo ambayo tumeleta hapa. Tulikuwa na watu wasomi, wakulima na pia watu wa serikali. Mimi ninaomba kuwa Seneti ikubaliane na maoni yetu ndio tuweze kuona vile tutakavyosaidia mkulima wa miwa ambayo inatengeneza sukari. Tukienda upande ule mwingine, katika Seneti, tumepitisha mambo mengi kwa mfano mambo ya ndengu kule mashinani, na hata sasa tuko na Mjadala wa Sukari na pia tumeongea mambo ya majani. Kwa hivyo, hakuna tofauti ya mkulima wa majani na mkulima wa kahawa na vitu vingine. Ninaunga mkono nikiomba Seneti yote ikubali maoni ya Kamati ya Kilimo ndio tuweze kusaidia mkulima. Tukiskia Maseneta wengine wakikuja hapa kusema kuwa hawakuhusishwa ni kitu cha aibu sana. Ni bora tu wasome ili tuweze kuona itakavyokuwa. Huenda ikawa mtu aliitwa lakini vitu hivyo vilikuwa kwenye mitandao na pia watu wengine walisema walipiwe ndege, ilikuwa jambo la aibu sana. Ninaomba Seneti iunge mkono na iwapo kuna mahali ambapo kuna shida juu ya kilimo, tutaomba tukae chini tesemezane ili tuone pahali tutatatua. Asante Bw. Spika."
}