GET /api/v0.1/hansard/entries/1398635/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1398635,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1398635/?format=api",
"text_counter": 285,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda. Nimesimama siku ya leo kujiunga na Kiongozi wa Walio Wengi na pia Kiranja wa Seneti, kuunga mkono Mswada ulio mbele yetu. Kwa muda mrefu, wananchi wengi wamekuwa wakikosa huduma katika ofisi nyingi kwa sababu ya ukosefu wa maadili na pia ufisadi. Kwa hivyo, sheria kama hii ni muhimu sana ili kuhakikisha kwamba wanaotafuta huduma kwa zile ofisi, wanapata huduma bora, pasipo ubaguzi kwa sababu hawajulikani au hawachukuliwi kama wahusika wakuu katika zile ofisi. Bw. Spika wa Muda, siku ya leo, ukienda ofisi nyingi, utapata wale wanaotafuta ajira au kazi ni lazima wawe na uhusiano fulani na mwenye yuko kwa hio ofisi. Kwa hivyo, ile sheria itakayotokea kutoka kwa huu Mswada itakua muhimu sana ili kuhakikisha ya kwamba maadili yanahifadhiwa na watu wanapewa heshima; na Wakenya pia, wanapata huduma kwa njia inayofaa. Asante."
}