GET /api/v0.1/hansard/entries/1398887/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1398887,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1398887/?format=api",
    "text_counter": 242,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika wa Muda. Swali langu ni kuhusu kupotea kwa umeme katika Kaunti ya Mombasa haswa wakati huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhan. Limekuwa jambo la kawaida umeme kupotea mara kwa mara katika Kaunti ya Mombasa na maeneo ya karibu haswa tunapokuwa tunafanya ibada za usiku. Wengi wanashindwa kuhudhuria ibaada hizo kwa sababu ya ukosefu wa umeme na vile vile kiusalama si rahisi mtu kutoka nyumbani ikiwa mataa barabarani yamezimika kwa sababu ya ukosefu wa umeme. Je, waziri ana mipango gani ya kuhakikisha kuwa kwa siku 14 ambazo zimebaki za mwezi huu mtukufu tutakuwa na umeme na sio katika Kaunti ya Mombasa pekee, lakini nchi nzima ili waisilamu wapate uwezo wa kumuomba Mungu wao bila matatizo yeyote? Asante."
}