GET /api/v0.1/hansard/entries/1398978/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1398978,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1398978/?format=api",
"text_counter": 333,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda. Nashukuru Waziri pamoja na Katibu wa Kudumu, Mhe. Alex Wachira, kwa kazi nzuri ambayo wanafanya. Tunaona yanayofanyika mashinani bila kelele. Ningependa kumkumbusha kuwa kuna Kauli niliyoagiza awali kuhusu stima ambayo ilikuwa inawekwa Gichugu mahali panaitwa Gitemani, kwani imekaa kwa muda mrefu bila kuwekwa. Kuna wananchi kama 700 ambao watafaidika. Mipaka imewekwa na ningeomba waziri aangalie suala hili, ili litekelezwe haraka na kusaidia wakaazi hawa. Mwisho ni kuhimiza kuhusu mikakati ya kuweka nguvu zinazotumia solar katika sehemu ukulima unafanyika kama Tana River. Wakulima wanatumia nguvu za stima ili kunyunyuzia mimea maji. Hii inaweza kupunguza gharama kwa wakulima, ili wapate pesa mfukoni kama vile Serikali hii ilivyopanga."
}