GET /api/v0.1/hansard/entries/1399184/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1399184,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1399184/?format=api",
    "text_counter": 174,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii. Nimesimama kuambatana na Kanuni ya Kudumu 52(1) kutoa kauli ya jumla kuhusu suala muhimu la kitaifa kuhusu hali ya usalama katika Kaunti ya Laikipia. Hali ya usalama katika Kaunti ya Laikipia imekuwa ya kutatanisha, hasa katika kipindi cha wiki moja iliyopita. Visa vya kutishia hali ya usalama katika Kaunti ya Laikipia vimekuwa vikiongezeka kadri siku zinavyopita. Kisa cha hivi punde ni kile kilichotokea usiku wa jana, tarehe 25 Machi, 2024. Wezi walipovamia Kata ya Yethi katika eneo la Daiga, Wadi ya Mukongondo mashariki katika Kaunti ndogo ya Laikipia Kaskazini. Katika kisa hicho, wezi waliokisiwa kuwa tisa waliiba na kutorosha ng’ombe wanne na mbuzi 30, mali ya Bw. Martin Mugi Wangai, Chifu wa Kata ya Yethi, pamoja na jirani yake Bw. Boniface Muriithi. Siyo hayo tu, walimshambulia Bw. Muthoga wa Karuiru, kumchapa kichapo cha mbwa na kumuacha hali mahututi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}