GET /api/v0.1/hansard/entries/1399185/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1399185,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1399185/?format=api",
    "text_counter": 175,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Hali hii ya utovu wa usalama inazua hofu miongoni mwa wakazi wa Kata ya Yethi na maeneo jirani, hasa ikizingatiwa visa hivi vya utovu wa usalama vinazidi kukithiri kila uchao. Inatia hofu zaidi, visa vya utovu wa usalama vikiwalenga maafisaa wanaotarajiwa kuisaidia Serikali kuu katika utekelezaji wa usalama mashinani kama vile machifu. Wakazi wanadai kuwaona wezi hao wikitokomea porini. Licha ya polisi kuwa andamana wezi hao kwa magari maalum ya vyombo vya usalama na ndege ya Ranchi ya Borana kutoa usaidizi wa angani kuwatafuta wezi hao, hawakuwapata. Hatimaye jioni saa tatu kasoro dakika kumi walishambulia chifu na kumuibia mifugo yake. Ikiwa chifu atalengwa katika mashambulizi ya aina hii, basi ni dhahiri kuwa usalama umedorora sana na raia hawapo salama kamwe. La kusikitisha zaidi ni kwamba shambulizi hilo la hivi punde katika Kata ya Yethi lilifanyika katika makazi yalio karibu sana na kituo cha polisi ila polisi hawakuwakabili kwa dharura. Nikihitimisha kauli yangu, ningependa kuvisihi vyombo ya kitaifa vya usalama kukabili hali hii ya utovu wa usalama katika kaunti nzima ya Laikipia ili kuwahakikishia raia uhuru wa kuendelea na shughuli zao za kila siku pamoja na usalama kama ilivyonakiliwa kwenye Katiba ya nchi. Hasa ningependekeza maafisa zaidi wa vitengo mbalimbali vya kudumisha usalama kuelekezwa kwa dharura kushika doria nyakati za usiku katika maeneo yaliolengwa sana na wizi wa mifugo na visa vyovyote vile vya ukosefu wa usalama katika Kaunti ya Laikipia. Kwa kufanya hivyo, wakazi wa Kaunti ya Laikipia watahisi kuwa vilio vyao vimesikizwa na hatua kuchukuliwa. Rumuruti kulishambuliwa vijana wawili walipokuwa wakitoka kanisani na kuuwawa papo hapo. Kwa hivyo, tunahitaji usalama."
}