GET /api/v0.1/hansard/entries/1399228/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1399228,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1399228/?format=api",
    "text_counter": 218,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chimera",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante sana Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii niweze kuchangia katika mjadala wa swala hili lote la Mswada huu wa boundaries za kaunti zetu. Kwanza nianze kwa kumshukuru sana na kumpongeza kaka yangu Sen. M. Kajwang kutoka Kaunti ya Homabay kwa Mswada huu. Nafikiri ni wazi kwamba Mswada huu ni wa maana sana katika hali hii yetu ya kauti zetu katika nchi hii. Nafikiri unafahamu ya kwamba kaunti tofauti tofauti ziko katika hali ya migogoro hususan kuhusu swala la mipaka. Mimi mwenyewe nikiwa Seneta kutoka Kaunti ya Kwale na nikiwa wakili vile vile, niko mahakamani ninapo zungumza hapa kwa niaba ya wananchi wa Kijiji cha Kanjaocha katika Wadi ya Samburu Chengoni eneo ubunge la Kinango Kaunti ya Kwale, wakizozana na Kaunti ya Kilifi kuhusu mpaka baina ya Kaunti ya Kwale na Kilifi. Vile vile, nikizungumza hapa, Kaunti ya Kwale ina mgogoro ambao umekithiri kwa wingi. Kaunti ya Taita-Taveta imeweza kuvamia ule mji wa Mackinon. Mimi tangu nizaliwe, na sitaki kusema umri wangu lakini nimeishi kwa miaka mingi. Sio mingi vile The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}