GET /api/v0.1/hansard/entries/1399229/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1399229,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1399229/?format=api",
"text_counter": 219,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chimera",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "lakini sijaona siku hata moja Kaunti ya Taita-Taveta imeweza kuja Mackinon na kusema ule ni mji wao. Lakini leo hii, Gavana wa Kaunti ya Taita-Taveta, Mheshimiwa na mjomba wangu na pia rafiki yangu sana, Mhe. Andrew Mwadime, kwa kejeli na majivuno na kwa kujigamba, ameweza kuvamia mji wa Mackinon na kuchukua kodi kwa wafanyibiashara mbalimbali kutoka Kaunti ya Kwale. Nimeona kwa First Schedule ya Mswada huu kwamba Kaunti ya Kwale ukiangalia sehemu ya pili imesema kwa kifupi kwamba Kaunti ya Kwale imeanzia upande wa kushoto katika kona ya Mackinon Road. Hii ni wazi kwamba Mswada huu umeweza kuleta mfumo wa kisheria. Sisi kama viongozi katika kaunti tofauti tofauti, tukiwa na swala la mjadala kuhusu mipaka ya kaunti, tunaweza kurudi kwa sheria tukaipekuapekua na tukapata mwongozo au ufahamu ni jinsi gani tutatatua swala hili. Mimi tu nisiseme mengi kwa sababu nafikiri wenzangu wamezugumzia mengi sana kuhusu Mswada huu. Nizungumzie kwa kifupi kuhusu hii kamati ambayo imewekwa katika sheria hii, Kamati ya Mediation . Nimeona kama imepewa nguvu nyingi zaidi. Nimrai tu kakangu Sen. M. Kajwang pengine kuna haja ya kupiga msasa Mswada huu kuhakikisha ya kwamba yale mapendekezo ya kwamba kaunti yoyote inaweza kuruhusiwa kubadilisha mipaka yake, yasikuwe pale katika sheria hii kwa sababu itazidi kuleta migogoro zaidi. Kutakuwa na chuki baina ya kaunti tofauti tofauti na tunajaribu kupata suluhu ya kudumu. Niweze tu kusema kwa kifupi kwamba mimi ninaunga mkono Mswada huu. Nawauliza Maseneta wenzangu, ingekuwa vyema kama Mswada huu ungekuwa wa Kiserikali ndio tuweze kufanya haraka, tuupitishe kwa haraka, ili tupate suluhu ya kudumu katika kaunti zetu hizi za Kwale na Taita-Taveta; Taita-Taveta na Makueni, hata Kaunti ya Kericho na Kisumu waweze kuwa na mfumo wa kisheria ambao watatumia kutatua mgogoro huu. Mimi naunga mkono Mswada huu. Asante Bw. Spika wa Muda."
}