GET /api/v0.1/hansard/entries/1399281/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1399281,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1399281/?format=api",
"text_counter": 271,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, sukari imekuwa tamu kwa wenye wanaitumia lakini imekuwa chungu kwa wakulima. Wakati tumekuwa tukizunguka kama Kamati ya Ukulima, Uvuvi, Mifugo na Uchumi Samawati, katika maeneo yanayokuza sukari, tumejionea wakulima ambao wamenyanyaswa na kuteseka kwa muda kwa sababu ya sharia na usimamizi mbaya wa kampuni za sukari nchini. Mswada uliotufikia kupitia mdhamini Sen. Wafula, ulifanya tuzuru mashinani na kuongea na wakulima wenyewe kama ilivyo kawaida yetu. Tulienda katika maeneo ya Busia, Bungoma, Kakamega hadi Chemelil katika Kaunti ya Kisumu. Tulipokea nakala kutoka kwa wakulima wa miwa kutoka Kaunti ya Kwale pamoja na malalamishi yao. Nawashukuru Maseneta wote tuliyo shirikiana nao katika safari ile, akiwemo Sen. (Dr.) Khalwale, Sen. Wafula, Sen. Okiya Omtatah, Sen. (Prof.) Tom Odhiambo Ojienda, SC, na pia wale wengine kama Sen. Sifuna aliyekuwa anafuatilia kwa kina na ukaribu Mswada huu wa kunufaisha wakulima wa miwa. Bw. Spika wa Muda, ukiona majonzi yaliyokuwa na wakulima hawa walipokuwa wanahudhuria vikao vya kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Seneti, ili kujieleza, ungejua kuwa wakulima wa maeneo yale wametatitizika kwa muda. Wakulima kutoka kaunti za Nandi na Kericho walikuja Chemelil ili kuyawasilisha maoni yao hawajasahaulika kwa sababu ya shida zilizokuwepo. Sitakawia kueleza lakini niruhusu kusema haya. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}