GET /api/v0.1/hansard/entries/1399282/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1399282,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1399282/?format=api",
"text_counter": 272,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Vyama vya ushirika vya kusaga miwa kama Nzoia Sugar hawajawalipa wafanyikazi mishahara yao ilhali miwa inavunwa na kupelekwa katika viwanda hivi. Hili ni jambo la kutia hofu. Tuliweza kuweka zoning kwa mipaka ili tuangalie mahali ambapo miwa inapelekwa na pia kwenye uchaguzi wa wanaosimamia ukulima wa miwa. Katika bodi ya Sukari, Seneti hii ilihakikisha kuwa wakulima wana waakilishi wengi zaidi ili malalamiko ya wakulima itatuliwe na kama kuna upigaji kura katika jambo linalotokea sauti ya mkulima itasikizwa. Bw. Spika wa Muda, baada ya miwa kusagwa na sukari kuuzwa, kuna matokeo ya pembejeni ambayo inabaki katika mitambo kama “sukari nguru” na vinginevyo ambavyo hutumika kutengeneza chakula cha ng’ombe na husaidia uchumi wa nchi hii. Wakulima walilalamika kuwa wanapouza mabaki haya, pesa zile haziwafaidi kamwe. Mswada huu unafaa kutatua mambo kama yale. Usafirishaji wa miwa kutoka eneo moja hadi lingine lazima udhibitishwe. Mswada huu unaelekeza kuwa tutauwa vyama hivi vya ushirika na wale wanaopeana pembejeo kwa wakulima. Mkasa uliopata kiwanda cha Nzoia Sugar ulisema kuwa kuna wakulima waliopewa pembejeo, wakalimiwa shamba lakini baadaye wakachukua miwa na kuuzia wasiohusika kamwe katika upanzi wa miwa ile. Nzoia Sugar ilipata deni ya milioni Kshs900, ikasambaratika na wakulima wakaumia. Mgala muuwe na haki yake mpe. Kama tutakuwa na nchi nzuri ambayo ina maendeleo katika kila kona, lazima tuhakikishe kuwa magatuzi yote 47, yatapata nafasi ya mimea ambayo itawapa pesa. Ndio maana Kamati hii imejitahidi sana na kuleta Miswaada ya Pamba, Ndengu na Kahawa ambayo ilipitishwa na Maseneta. Naomba kwamba, mwisho wa wiki hii tutaupitisha Mswada huu wa sukari, ili tuwasaidie wakaazi na wazaliwa wa nchi hii. Asante."
}