GET /api/v0.1/hansard/entries/14008/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 14008,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/14008/?format=api",
"text_counter": 434,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Mhe Naibu Spika, nashukuru kwa nafasi hii ili nichangie Hoja hii. Ninamwomba Waziri wa Matibabu katika nchi yetu asikie kilio cha Wakenya. Sauti ya mwananchi ni sauti ya kiongozi, na sauti ya kiongozi ni sauti ya Mungu. Bw. Naibu Spika, nimefurahishwa na wenzangu ambao wamechangia Hoja hii kwa sababu hawajazungumzia mambo ya ukabila. Hawazungumzii mtu awe wa sehemu fulani. Ninafurahi kwa sababu wanasema kwamba hata kama mtu anatoka pembe gani ya nchi hii, kama ana uwezo, anastahili kupewa nafasi kuongoza kituo kile cha matibabu. Ningetaka Waziri aelewe kwamba wakati anaulizwa kuvunja Bodi ilioko kwa sasa ni jambo limefikiriwa kwani wanaochangia sio wendawazimu. Wanaochangia ni watu ambao wanaitakia nchi hii mema. Imedhihirishwa hapa kwamba hasa wanaotoka karibu na ile hospitali wameweza kushuhudia na kuona kwamba kweli kumetokea mambo ambayo hayawezi kukubalika katika uongozi wa hospitali hiyo. Ni aibu na ninashindwa kutaja jina la mtu. Lakini aliyeteuliwa kama Kaimu Mkurugenzi wa hospitali ile, Waziri afahamu kwamba tumetoka kwa mipango ya zamani tulipokuwa tunasema kwamba mtu fulani anateuliwa kupitia mlango wa nyumba. Waziri ni mtu amepigania mabadiliko katika nchi hii na yale yanahitajika kufanyika aliyapigania yeye mwenyewe. Bw. Naibu Spika, awali ni mmoja tu. Lakini tunataka Wakenya watume maombi yao ili wahojiwe kwa kazi ya Mkurugenzi wa hospitali hiyo. Baada ya kuhojiwa, tunataka Bodi iwasilishe majina ya watu watatu kwa Rais ili amteue mkurugenzi wa hospitali hiyo. Hatutaki jambo hili lilete kasheshe. Ninamuuliza Waziri afanye jambo hilo kwa haraka ili awapatie Wakenya mwongozo wa kuenda mbele. Hii ni mojawapo wa kielelezo ambacho kitaweza kufuatwa baadaye. Ikiwa Waziri hatafaulu kwa jambo hili, basi litatumika katika Wizara nyingine na tutahama katika mabadiliko ya Katiba mpya na kuenda kwa mambo ya zamani. Tutaanza tena kujiuliza kama tunafanya kazi kulingana na Katiba mpya ama Katiba ya zamani. Kwa hivyo, tukubali watu watume maombi yao kwa Bodi ili tupate uongozi mpya katika hospitali hiyo. Ukifanya hivyo, tutakupa heshima kubwa na Wizara yako itaheshimika. Kama kumetokea maafa ya watu na imeweza kuthibitishwa, ni jambo gani lingine linangojewa na kutarajiwa kuzungumziwa? Ningetaka Kenya iwe nchi inayoongozwa na Katiba na Katiba ijaribu kutumiwa inavyowezekana ili tuweze kuondoka katika mambo ya kulaumiana, kukashifiana na kujionyesha kwamba hatuna kazi ambaoyo tunaweza kufanya. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}