GET /api/v0.1/hansard/entries/1400906/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1400906,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1400906/?format=api",
    "text_counter": 67,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Miraj",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika, nami pia namkaribisha Waziri. Kule Mombasa kuna Uhuru Gardens. Hapo awali, sehemu hiyo ilikuwa imenyakuliwa na mabwenyenye. Tunashukuru kwa sababu tulirejeshewa hatimiliki. Kama mwakilishi wa Mombasa, je, tunaweza kupata huduma kama zile zilizoko katika Kaunti ya Nairobi? Kunaweza kuwa na marekebisho ama ukarabati ili kurejesha nidhamu? Kuna changamoto kubwa ambayo inatukabili kule Mombasa. Kuna jamii za watu wanaorandaranda ambazo zinaongeza idadi ya utovu wa usalama katika mji wetu. Labda tukipewa fursa, tunaomba mje pale mturekebishie ili kuwe na nidhamu kwa sababu imekuwa kero kwa wananchi wa Mombasa pale Uhuru Gardens na Makadara Grounds. Je, tunaweza kufanyiwa ukarabati wa bustani zetu? Vile vile, ningependa kukuomba kwa sababu unahusika katika sekta ya usalama. Tafadhali mtafute mbinu ya kushirikiana na Gavana wetu wa Mombasa ili watu wapate makazi mazuri. Sitaki nieleweke vibaya kwamba tunataka kuwaondoa, lakini sio The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}