GET /api/v0.1/hansard/entries/1400974/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1400974,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1400974/?format=api",
"text_counter": 135,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Shakila Abdalla",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 380,
"legal_name": "Shakila Abdalla",
"slug": "shakila-abdalla"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Kwanza ningependa kuchukua nafasi hii kumpongeza Waziri kwa utaalamu wake wa kujibu maswali. Bw. Spika, nimeona ameguzia juu ya mambo ya ugaidi Lamu. Ningependa kumueleza kwamba kuna barabara ya Lamu-Kiunga ambayo haipitiki na inachangia pakubwa sana kwa kuwasaidia watu ilhali hiyo ndio barabara inayotumika na magaidi. Mara nyingi utakuta wakaazi wa Kiunga wanatumia njia ya bahari kwa sababu ya ukosefu wa usalama wa barabara ya Kiunga kwenda Lamu. Naomba Mhe.Waziri, kama kuna uwezekano wa majeshi kwenda kuirekebisha ili ikupunguza ugaidi na kuimarisha usalamu katika Kaunti ya Lamu. Ninajua Bw. Waziri ni muhusika mkubwa katika Wizara yake juu ya usalama, hiyo barabara inachangia pakubwa na ninajua yeye anaelewa vizuri mambo ya ugaidi yanayotuathiri katika Kaunti yetu ya Lamu. Bw. Spika, ingekuwa vyema kama Waziri angeweza kulijibu hili swali na atuhahakikishie kama kuna uwezekano wa majeshi kuja kurekebisha barabara hii ya Lamu-Kiunga. Asante."
}