GET /api/v0.1/hansard/entries/1401069/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1401069,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1401069/?format=api",
"text_counter": 230,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu wa Spika. Langu ni kumuuliza Bi. Waziri kwamba kuna malimbikizi ya malipo kwa zahanati na vituo vya afya ambayo yameendelea kwa muda mrefu. Na majibu yake hayajaridhisha kwa sababu hajasema pesa zinazodaiwa ni ngapi na zitalipwa vipi. Tumeona, wakati NHIF ilipokuwa inafanya kazi, malipo yalikuwa hayaendi na sasa tunatoka katika NHIF na kuenda kwa shirika jipya. Tunataka ueleze Seneti hii kwanza madeni ni pesa ngapi. Pili, una mipango gani ya kulipa madeni hayo? Unaposema ya kwamba yatalipwa hayo ni mambo ya Alfulelaulela."
}