GET /api/v0.1/hansard/entries/1401868/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1401868,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1401868/?format=api",
    "text_counter": 641,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipa wakati huu nitoe mchango wangu kuhusu National Land Commission (NLC). Nampongeza ndugu yangu, Mhe. Owen Baya, kwa kuangalia historia hasa katika Ukanda wa Pwani. Hii Tume ya kuangalia mambo ya mashamba imekuwa ikisaidia sana kwa kutoa uwazi wa mambo yalivyo kule chini. Watu wetu wanateseka sana. Kwa mfano, baada ya Tume hii kuangazia dhuluma za kihistoria za mashamba, kuna watu mpaka sasa wanahangaishwa. Ni dhahiri shahiri kuwa Tume hii ilichaguliwa na kutengwa ili isaidie historia ya dhulma za mashamba na mambo kama hayo ili mnyonge aweze kupata haki yake. Sasa hivi tunavyozungumza, hata sisi pia tumeleta malalamishi ambayo yametoka katika kaunti zetu. Ukanda wa Pwani umekuwa ndio chanzo kikubwa cha kupata dhuluma za kihistoria za mashamba. Watu wetu wamekaa kama maskwota, na ukiangalia katika mashamba yale, kuna watu wamekaa zaidi ya miaka 200. Lakini, ile dhuluma wanafanyiwa, hasa ukiangalia wakazi wa pale Majengo, Mwembe Kuku, Bondeni na Kisiwani, bado wanalalamika na mpaka sasa hawajapata haki yao. Hii Tume ikiwekewa muda rasmi, itakuwa haina mwanya wa kujieleza zaidi. Hawa watu wamekaa zaidi ya miaka 200 kwenye shamba. Ukiangalia mpaka sasa, wanaambiwa watafurushwa kwenye mashamba yao. Mtu anajitokeza tu. Yeye amepotea na amekaa nje miaka yote. Lakini, anakuja kunadi na kuwapatia wale wazee wasiwasi, akiwaambia atawavunjia nyumba zao waondoke, wakati wamekuwa wakilipa kodi kwa zaidi ya miaka 50. Sheria iko wazi kuwa Wakenya wapewe ithibati ama hati miliki za mashamba ndio wakae kwa amani. Lakini, unapata kuna watu wanawanyanyasa, ndio maana Tume hii iliwekwa ili kuangalia maswala hayo. Naunga mjadala huu mkono ili Tume hii ikae na iwekwe wazi bila vizingiti vya miaka mitano, ndio tupate kutatua shida ambazo Wakenya wanapata. Napatia hii Tume ya Mashamba changamoto wafanye kesi nyingi, kwa sababu wamesikia mambo mengi ya mashamba na vilio vya watu wengi. Mpaka sasa, wamefanya kitu gani kuhakikisha kuwa watu wetu wanapata haki zao? Hii Tume ni nzuri sana, lakini naomba iweze kutatua matatizo yaliyoko ili Wakenya wapate haki zao. Kama tunavyoona wazee wetu, Council of Elders au Baraza la Wazee kule Mombasa wamelia sana. Mzee Sumba amelilia mashamba mpaka amezeeka, umri umekwenda, The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"
}