GET /api/v0.1/hansard/entries/1401869/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1401869,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1401869/?format=api",
"text_counter": 642,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "lakini anatoa machozi kwa sababu wanavunjiwa manyumba katika mashamba wakati Serikali imenyamza. Namwambia ndugu yangu, Owen Baya, kwamba sote tumetoka Pwani, na tunajua matatizo ya watu wetu. Ndugu yangu uko katika mrengo wa Serikali, na naomba uingilie kati. Tunaitetea Tume ya Kitaifa ya Mashamba waweze kujibidiisha na kupigania haki za wanyonge, ili hao ndugu zetu waweze kupata title deeds na kukaa kwa amani. Wakati mwingine nikikaa huwa nalia machozi nikiona vile watu wangu wanavyodhalilishwa. Makaburi ya wazee mahali ambapo wamelala, wanahangaishwa. Mtu anatoka kule Oman na anakusanya rent ndani ya Mombasa ilhali, nchi yake ni nyingine. Naiomba Tume ya Kitaifa ya Mashamba waangazie Serikali na kuiambia hawa ni Wakenya wazaliwa, hata kama ni wanyonge na hawana pesa za kwenda mahakamani kujitetea. Lakini, Serikali itoke kuwatetea wanyonge, ambao ni Wakenya, wapate haki yao. Naunga mkono mjadala wa leo nikisema kuwa Tume ya Kitaifa ya Mashamba iwachwe ifanye kazi bila kuwekewa vizingiti vya wakati. Lakini, ijibidiishe kutoa matukio ambayo wamepata. Pia, watupatie udhabiti kuwa walisikiliza vilio vya watu fulani, wametatua na wakapata hati miliki za mashamba. Pengine mtu alipokonywa shamba lake, aweze kuregeshewa hilo shamba. Wasiwe wanakaa tu Nairobi na kuwaambia watu waje na wakija wanalala kwa mahoteli. Hatuwezi kukubali, kwa sababu hawana pesa, na kisha wanabaki hivyo hivyo. Wawajibike kama Tume ya Kitaifa ya Mashamba, kuhakikisha kuwa wanapatia watu wetu haki zao; na waonyeshe matokeo ya kazi waliyopewa, japokuwa wanalipwa na Mkenya yule wa chini. Naunga mkono nikisema Tume ya Kitaifa ya Mashamba isitolewe, isisitishwe, wala isiwekewe mipaka. Iwachwe huru. Miaka nenda miaka rudi, tuwe nayo, iwe inasaidia Wizara ya Ardhi kufanya kazi. Pale Ardhi House kuna uozo mkubwa sana. Leo tukisema tunawaachia wao ndio wachukue kila kitu wafanye, mtu ambaye amekaa ndani ya nyumba yake miaka 50 ama 100, ataskia mtu amekuja na hati miliki, akisema pale ni kwake. Uozo huu uko pale Ardhi"
}