GET /api/v0.1/hansard/entries/1402419/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1402419,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1402419/?format=api",
"text_counter": 176,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": "Kama ilivyopendekezwa katika huu Mswada ambao ninaunga mkono, ni jambo la kuhuzunisha kwamba biashara inakuwa ngumu kufanya. Wakati mwingine hata sio biashara tu, hata usafiri. Lori ambalo hata halijabeba kitu likipita kaunti moja hadi nyingine imekuwa ni kama kupitia nchi moja mpaka nyingine. Kwamba, lazima liwe na vibali vya kaunti ambako linaenda licha ya kutozwa ushuru wa ule mzigo ambao limebeba. Hivi vibali ambavyo kaunti zinatoa kwa magari ya mizigo si halali. Tunajua kuwa katika nchi hii, tunayo Wizara inayohusika na kutoa vibali nayo ni Wizara ya Uchukuzi. Na kama ni insurance basi inakua ni ya Kenya nzima. Lakini kaunti zingine zimeweza kutoa vibali vya kadi na kubandika katika magari, kuonyesha gari hili linaruhusiwa kufanya biashara katika eneo lao. Jambo hili halina msingi, bali ni hali ya kuhangaisha wanabiashara. Ni hali ya kufanya bidhaa ziwe ghali zaidi ilhali tunazungumzia ni vipi wananchi wa kawaida wanaweza kupata afueni kibiashara. Nchi hii ni moja na kaunti zililetwa kwa sababu ya kupeleka huduma mashinani. Lakini saa hizi zimekuwa zikiwafinya watu kupitia hizi sheria zao. Kutoka maeneo ya Kwale kuingia Mombasa ni kama ambaye unavuka mpaka wa Lunga Lunga kutoka Kenya kwenda Tanzania. Kwa hivyo, Mswada huu ni muhimu na unahitaji kuungwa mkono na kupitishwa haraka inavyowezekana ili biashara zifanywe bila matata ama pingamizi yoyote."
}