GET /api/v0.1/hansard/entries/1402420/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1402420,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1402420/?format=api",
"text_counter": 177,
"type": "speech",
"speaker_name": "Matuga, ANC",
"speaker_title": "Hon. Kassim Tandaza",
"speaker": null,
"content": "Mhe. Naibu Spika, jambo jingine ambalo ni la kuhuzunisha ni ufadhili. Kwa mfano, pale Kaunti ya Kwale labda ufadhili utapitia Bandari ya Mombasa ambayo ni kaunti nyingine. Kwa mfano, mtu amenuia kusaidia shule za Kwale kwa kuzipa kompyuta ama vitu ambavyo vitatumika katika darasa. Kisha gari linapofika mpakani kati ya Kaunti ya Mombasa na Kwale pale Likoni yule mfadhili analazimika kulipa ushuru tena licha ya kuwa pengine ashalipa kwa Serikali kuu bandarini. Kaunti bado inahitaji ushuru tena ulipwe ili vyombo viweze kuingia ilhali bidhaa si za biashara - ni mtu binafsi amejitolea kutoa ufadhili kusaidia watu wetu. Lakini yule afisa ambaye amewekwa pale kwenye kituo cha cess anashauri kwamba ni lazima gari lolote linalopita hata ingawa ni la ufadhili lilipe ushuru la sivyo atalifungia. Inabidi mwenye gari azungumze na mstahiki gavana ama mkubwa ambaye anahusika, ili gari liachiliwe. Sisi kama Bunge tuna jukumu la kuona kwamba hali tata kama hizi haziwezi kuendelea. Ikiwa watatoza ushuru basi mtu akiwa ametoka Kilifi akienda Kwale, akilipa ushuru Kaunti ya Kilifi, aweze kubeba risiti kuonyesha tayari ashalipia katika gatuzi moja na anastahili kuubeba mzigo mahali popote pale Kenya. Hii ni kwa sababu nchi ni moja. Alikotoa bidhaa yule mfanya biashara amelipishwa, pengine, Ksh200 na akifika Mombasa analipishwa Ksh800. Akivuka Kwale analipishwa labda Ksh1,000. Je, atapataje faida yake?"
}