GET /api/v0.1/hansard/entries/1402562/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1402562,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1402562/?format=api",
"text_counter": 61,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Lakini fursa hii imekuwa ni sababu ya baadhi ya mashirika yanayo faidi kutokana na mpago huu kukandamiza haki za wafanyikazi, hivyo basi kuhujumu sekta hii ambayo inatoa ajira kwa Wakenya wengi. Kumekuwa na visa tele vya ukandamizaji wa haki za wafanyikazi mikononi mwa mashirika haya kama ifuatavyo - (i) Kuzuiliwa kwa wafanyikazi kujiunga na chama cha kutetea haki zao na kupelekea waliojiunga na vyama hivyo kupoteza kazi zao; (ii) Hujuma za kijinsia ambazo kina dada wanalazimishwa kushiriki tendo la ngono na waajiri au wasimamizi wa kampuni ili kupata ajira; (iii) Kufanyishwa kazi kwa muda mrefu bila kupewa barua za uajiri; iv) Ubaguzi na ukabila ambapo jamii moja pekee ndio inafanya kazi katika kimoja maalum kwa kampuni hiyo; v) Kufanyishwa kazi kwa muda mrefu katika mazingira duni yenye msongamano na vumbi, kupelekea afya za wafanyikazi kuwepo hatarini na kupata magonjwa; vi) Mishahara duni inayolipwa na mashirika hayo, basi kunyanyasa Wakenya; na pia, Vii) Hali tete iliyopo katika mashirika haya ambapo wafanyikazi hawajui hatima ya siku za baadaye. Majuzi wafanyikazi wa Kampuni ya Ashton Apparels iliyoko katika eneo Bunge la Changamwe mjini Mombasa walifanya mgomo kutetea haki yao ya kujiunga na chama cha wafanyikazi. Wafanyikazi hao walitimuliwa na maafisa wa polisi wakisaidiwa na Naibu Kamshna wa Kata Ndogo ya Changamwe bila ya kuwa na kosa lolote. Licha ya viongozi wa Mombasa kuingilia swala hilo, shirika limekataa kukubaliana na wafanyikazi, hivyo basi kupelekea wafanyikazi 2,000 kusimamishwa kazi. Serikali ya Marekani inazingatia kwa makini haki za wafanyikazi. Iwapo swala hili halitatatuliwa kwa haraka, Kenya iko hatarini kupoteza fursa hii ya mpango wa AGOA ambao ni muhimu vilevile kwa uchumi wa taifa. Tayari nchi kadhaa za Bara Asia zimepoteza fursa hii kwa sababu ya kutozingatia haki za wafanyikazi. Hili swala ni zito. Ninapendekeza Kamati ya Kudumu ya Leba na Ustawi wa Jamii ifuatilie ili wafanyi kazi wasidhulumiwe. Asante."
}